Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Imesasishwa:
Jibu fupi
Harusi Pass ni huduma ya kutuma kadi ya mwaliko kwa kila mgeni, kufuatilia majibu na michango, na kuingiza wageni langoni kwa QR au namba. Hapa kuna majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu gharama, usalama, michango na siku ya tukio.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Harusi Pass ni nini?
Ni huduma ya kutuma kadi ya mwaliko kwa kila mgeni kwa WhatsApp, SMS au karatasi, kufuatilia majibu na michango, na kuingiza wageni langoni kwa QR au namba, hata bila mtandao.
Inafaa kwa matukio gani?
Harusi, send-off, uchumba, kitchen party na sherehe nyingine za faragha. Unaandika aina ya mwaliko wewe mwenyewe.
Gharama ni kiasi gani?
Wakati wa majaribio ni bure. Gharama za SMS zinaonyeshwa kabla ya kutuma, na bei za baadaye zitatangazwa kabla ya kuanza kutozwa.
Je, wageni wanahitaji akaunti au programu?
Hapana. Wanafungua kiungo cha kadi yao kwenye simu. Wasio na smartphone wanapata SMS yenye namba au kadi ya karatasi.
Kadi inatumwa kwa njia gani?
WhatsApp, SMS au PDF ya kuchapisha. Unaweza kuchagua njia kwa kila kikundi cha wageni, na SMS inatumika kama mbadala ikiwa WhatsApp haikufika.
Michango inalipwaje?
Kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa kutoka kwenye kadi ya mgeni. Kamati inaweza pia kurekodi taslimu na benki.
Michango ni lazima ili mgeni apate kadi?
Hapana. Kwa chaguo-msingi hakuna sharti. Mwenyeji akitaka kuweka sharti, lazima ayawashe mwenyewe.
Itakuwaje mtandao ukikatika siku ya harusi?
Programu ya lango inahakiki QR kwenye simu bila mtandao na kusawazisha baadaye. Kadi ya mgeni pia inaonekana bila mtandao baada ya kufunguliwa mara ya kwanza.
Mtu akipiga picha ya QR ya mwingine?
Kila QR ni ya mgeni mmoja na inaingiza mara moja. Ikiskaniwa mara ya pili, kamati inaona nani aliingia na saa ngapi.
Kadi ikipotea au ikitumwa kwa mtu asiyestahili?
Mwenyeji anatoa kadi mpya kwa mgeni huyo; kadi ya zamani inakoma kufanya kazi.
Mlinda lango anahitaji nini?
Simu ya Android, kiungo cha lango na PIN kutoka kwa mwenyeji. Hapati taarifa za pesa.
Data za wageni zinalindwa vipi?
Tunakusanya kiwango cha chini kinachohitajika, hatuuzi data, na mwenyeji anaweza kuzipakua au kuzifuta. Soma sera ya faragha na ukurasa wa maombi ya data.
Mgeni anaweza kuomba data zake zifutwe?
Ndiyo. Anaweza kuwasiliana na kamati au nasi kupitia ukurasa wa maombi ya data.
Je, ni ulaghai? Nitajuaje kadi ni halali?
Kadi halali inaonyesha mtumaji na namba ya kamati, na haiombi nenosiri wala PIN. Soma ukurasa wa usalama wa kadi.
Mnafanya kazi nchi gani?
Imetengenezwa Tanzania kwa matukio ya Kitanzania, ikiwa na malipo ya simu ya Tanzania na Kiswahili kama lugha ya kwanza.
Tengeneza kadi ya kwanza bila malipo wakati wa majaribio.